Star Tv

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa Dkt. John Pombe Magufuli tayari amechukua fomu ya kuwania tena nafasi ya urais.

Rais Magufuli amechukua fomu ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama chake cha CCM.

Fomu hiyo ya kuwania urais aliyoichukua amekabidhiwa na Katibu Mkuu Dkt Bashiru Ally asubuhi ya leo Juni 17,2020 jijiji Dodoma.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, Rais Magufuli amesema ataanza mapema mchakato wa kutafuta wadhamini ili awahi kurejesha fomu hiyo ndani ya muda uliopangwa.

 “Naomba nianze zoezi hili la kutafuta wadhamini, nitaenda mikoa yote kwa sababu nimekuwa nikipigiwa simu wakisema wanataka kunidhamini hivyo nitarejesha fomu yangu kwa wakati,” amesema Rais Magufuli.

   Aidha, Rais Magufuli ameuthibitishia umma kuwa amekuwa akipigiwa simu na makada wa chama cha CCM ambao wamemuahidi kumdhamini katika kuwania tena kiti hicho cha urais.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.