Star Tv

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, amevamiwa na kushambuliwa na watu wasiojulikana wakati akirejea nyumbani kwake jijini dodoma.

Msemaji wa CHADEMA Tumaini Makene, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo lilitokea usiku wa Jumatatu, ambapo amevieleza vyombo vya habari kuwa kwa sasa anapokea matibabu.

Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika amevieleza baadhi ya vyombo vya habari kuwa shambulio hilo lina sura ya kisiasa, na amesema kuwa taarifa zaidi zitatolewa baadae.

Aidha, shambulio hili dhidi ya mwenyekiti wa CHADEMA linakuja siku moja baada ya mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu kutangaza rasmi nia ya kuwania urais kupitia chama cha CHADEMA.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.