Star Tv

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam, imemuachia huru Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe Leo Mei 29, kwa sharti la kwamba asitoe matamshi ya uchochezi katika kipindi cha mwaka mmoja.

Kesi hiyo ya uchochezi namba 327 ya mwaka 2018, Zitto alikuwa anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi, anayodaiwa kuyatenda Oktoba 28, 2018, wakati wa mkutano wake na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya chama hicho.

Katika shtaka la kwanza, ilidaiwa kuwa siku hiyo akiwa katika mkutano na waandishi wa habari alitoa naneno ya uchochezi yenye nia ya kuleta chuki miongoni mwa wananchi wa Tanzania dhidi ya Jeshi la Polisi.

Pia ilidaiwa kuwa Zitto Kabwe alizungumzia mauaji, yaliyotokea katika Kijiji cha Mpeta wilayani Uvinza mkoani Kigoma ambayo yalisababishwa na vurugu kati ya Polisi na raia.

Ikumbukwe kuwa kwa mara ya kwanza Zitto Kabwe, alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Novemba 2, 2018 kutokana na kesi hiyo.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.