Star Tv

Mkuu wa Jeshi ka Zimamoto na Uokoaji Kamishna Jenerali John Masunga amesema tayari wametekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kijana aliyesaidia katika shughuli za uokoaji kwenye ajali ya ndege ya shirika la presicion iliyotokea Novemba 06, 2022 wilayani Bukoba mkoani Kagera kwamba tayari wameshampokea Majaliwa Jackson Samweli kwa ajili ya kuanza mafunzo.

Masunga amesema kijana huyo anatarajiwa kuanza mafunzo ya Zimamoto na uokoaji pamoja na uaskari katika Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo Chogo wilayani Handeni mkoani Tanga.

Aidha Masunga ametoa wito kwa wananchi wote kuendelea kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika kuokoa maisha ya watu na mali dhidi ya majanga mbalimbali.

Latest News

Waziri Mkuu Akagua Visima Vya Dharura Dar Es Salaam
10 Nov 2022 13:31 - Kisali Shombe

¬†WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua visima vya dharura vinavyosafishwa, kufufuliwa na kuunganishwa katika mfumo wa us [ ... ]

Waziri Wa Afya Aagiza Udhibiti Magonjwa Ya Mlipuko
09 Nov 2022 14:15 - Kisali Shombe

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameagiza vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya binafsi na serikali kuweka kituo maalum  [ ... ]

Vifo vitokanavyo na Utoaji wa Mimba usio salama, Kudhibitiwa
09 Nov 2022 13:21 - Kisali Shombe

Mpango wa idara ya afya wa kutoa elimu ya afya ya uzazi na matumizi ya uzazi wa mpango unatajwa kusaidia kupunguza mimba [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2023 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.