Star Tv

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema kuwa Baraza la Mitihani ya Taifa limejiridhisha kwamba watahiniwa katika shule ya Chalinze Modern Islamic walibadilishiwa namba ya mtihani.

Kauli hii ya Waziri inakuja siku chache baada ya video zilizosambaa katika mitandao zikimuonesha mtahiniwa katika Shule ya Awali na Msingi Chalinze Modern Islamic Iptisum Suleiman Slim akilalamikia kubadilishiwa namba ya mtihani wa darasa la saba.

Prof. Mkenda amesema baada ya uchunguzi imebainika kuwa ni kweli mtahiniwa alibadilishiwa namba na kwamba pia watahiniwa wengine saba walibadilishiwa namba za mtihani.

Aidha kutokana na kukutwa na kosa hilo Serikali imeifungia shule hiyo kuwa kituo cha mitihani kwa muda usiojulikana kutokana na taarifa ya Kamati ya Mitihani ya Mkoa wa Pwani pamoja na taarifa ya Wataalamu wa Miandiko kutoka Jeshi la Polisi kubainika kuwa Watahiniwa 7 akiwemo Iptisam walibadilishiwa namba za mtihani katika Shule hiyo.

Mkenda amesema uchunguzi uliofanywa na Kamati ya Mitihani ya Mkoa wa Pwani umebaini kuwa Mtahiniwa Iptisam Suleiman Slim alifanya masomo matano kwa kutumia namba PS1408009/0040 na somo la sita (mwisho) kwa kutumia namba PS1408009/0039.

Latest News

Waziri Mkuu Akagua Visima Vya Dharura Dar Es Salaam
10 Nov 2022 13:31 - Kisali Shombe

¬†WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua visima vya dharura vinavyosafishwa, kufufuliwa na kuunganishwa katika mfumo wa us [ ... ]

Waziri Wa Afya Aagiza Udhibiti Magonjwa Ya Mlipuko
09 Nov 2022 14:15 - Kisali Shombe

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameagiza vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya binafsi na serikali kuweka kituo maalum  [ ... ]

Vifo vitokanavyo na Utoaji wa Mimba usio salama, Kudhibitiwa
09 Nov 2022 13:21 - Kisali Shombe

Mpango wa idara ya afya wa kutoa elimu ya afya ya uzazi na matumizi ya uzazi wa mpango unatajwa kusaidia kupunguza mimba [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2023 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.