Star Tv

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Angellah Kairuki amesema Serikali imetoa Shilingi bilioni 13.88 kwa ajili ya kuboresha huduma za afya katika Mkoa wa Kigoma.

Kairuki ameyabainisha hayo katika ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan kuzungumza na wananchi wa Mkoa wa Kigoma kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika.

Amesema kati ya fedha hizo zilizotolewa kwa mwaka 2021/22, Sh bilioni 6.6 zimetumika katika ujenzi na ukamilishaji wa vituo vya afya 15 na bilioni 1.2 zimeelekezwa kwenye ukamilishaji wa ujenzi wa Zahanati 24 katika Mkoa wa Kigoma.

Aidha pia amebainisha kuwa Sh bilioni 3.5 zilitolewa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali katika halmashauri 6 za Buhigwe, Kakonko, Kasulu DC, Kigoma DC, Kigoma MC na Uvinza DC.

Kuhusu miundombinu ya barabara, Kairuki amesema, Serikali imetoa Sh bilioni 21.7 kwa ajili ya kuimarisha barabara na imepanga kuitumia bilioni 34.1 kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Uboreshaji Miji (TACTIC) ambao umelenga kuboresha miundombinu katika Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Latest News

Waziri Mkuu Akagua Visima Vya Dharura Dar Es Salaam
10 Nov 2022 13:31 - Kisali Shombe

¬†WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua visima vya dharura vinavyosafishwa, kufufuliwa na kuunganishwa katika mfumo wa us [ ... ]

Waziri Wa Afya Aagiza Udhibiti Magonjwa Ya Mlipuko
09 Nov 2022 14:15 - Kisali Shombe

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameagiza vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya binafsi na serikali kuweka kituo maalum  [ ... ]

Vifo vitokanavyo na Utoaji wa Mimba usio salama, Kudhibitiwa
09 Nov 2022 13:21 - Kisali Shombe

Mpango wa idara ya afya wa kutoa elimu ya afya ya uzazi na matumizi ya uzazi wa mpango unatajwa kusaidia kupunguza mimba [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2023 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.