Waziri wa Madini Dokta Doto Biteko amefanya ziara ya kushtukiza katika soko la Madini mjini Geita ikiwa ni siku chache tangu kubainika kwa wizi mpya wa Madini ambao unapunguza ubora wa Dhahabu.
Akiwa katika soko hilo amesema wapo baadhi ya maafisa wanashiriki mchezo wa kupunguza ubora wa Madini wakishirikiana na wafanyabiashara na sasa wamekamilisha orodha yao hatua zaidi zitafata.
Dkt. Biteko ameongeza kuwa wanafanya operesheni Nchi nzima kufuatilia wanaodanganya juu ya ubora wa dhahabu na watakaobainika wanafanya hivyo watafutiwa leseni zao.