Chama cha Mapinduzi CCM kimewataka wanachama wake kutambua kuwa bila kujiimarisha kiuchumi kitakuwa na wakati mgumu wa kujiendesha hasa katika kipindi hiki cha kuelekeza uchumi wa kati.
Amesema hayo katika kongamano la vijana mkoani Manyara ambapo Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Manyara Paza Mwamlima ametumia fursa hiyo kueleza changamoto inayotakiwa kushughulikiwa na chama hicho ili kiweze kujiendesha bila kutetereka.
Katibu huyo amesema CCM bila kujiimarisha kiuchumu kupitia Jumuiya zake itakuwa vigumu kufikia malengo ya kuwa na uchumi imara. Aidha amewataka vijana kuwa mstari wa mbele kukemea vitendo viovu vinavyochangia kurudisha nyuma maendeleo ya chama.