Star Tv

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima ameitaka jamii kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wadau wote wanaosaidia kupambana na ukatili dhidi ya watoto likiwemo Jeshi la Polisi, Mahakama na Taasisi zinazojihusisha na uboreshaji wa huduma za Madawati ya Jinsia kwa kudhibiti ukatili dhidi ya watoto wadogo.

Amebainisha hayo katika ufunguzi wa kituo cha kulelea watoto cha pamoja cha huduma ya mkono kwa mkono kwa watoto waliofanyiwa ukatili katika Chuo Kikuu Kishiriki cha SAUT, Jordan kilichopo Morogoro kitakacho hudumia wakazi wa kata 15 katika Manispaa ya Morogoro.

"Tatizo la ukatili linaathiri maendeleo ya Taifa kwa kuwa na watoto watakaojifunza ukatili hali inayo ongeza mzigo kwa jeshi la polisi ambalo linafanya kazi kubwa ya kuanzisha madawati ya kijinsia kwa lengo la kuelimisha jamii itambue umuhimu wa kuzingatia maadili na malezi bora kwa watoto ili kuandaa taifa la vijana wazalendo kwa manufaa ya Taifa"- Amesema Dkt. Gwajima.

Dkt. Gwajima amevipongeza vyombo vyote vya sheria vinavyoshughulikia masuala ya ukatili na ametoa rai kwa vyombo hivyo vikiwemo polisi na mahakama kuongeza kasi ya kufanyia kazi mashauri ya ukatili ili kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake kwa wakati.

Mkuu wa Chuo Kishiriki cha Jordan Prof. Bertram Mapunda amesema kuwa chuo kimebaini mkoa wa Morogoro ukatili upo kwa kiwango cha asilimia 60 ambapo kila watoto 10 sita hufanyiwa ukatili wa aina mbalimbali ikiwemo ulawiti, Ubakaki, vipigo, kuunguzwa kwa maji na moto n.k. pindi watoto wanapokosea.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.