Star Tv

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amesema Serikali itatenda haki katika mchakato wa kuwapata washindi wa tuzo za filamu kwa mwaka 2021.

Waziri Bashungwa ametoa kauli hiyo katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Mbeya wakati akielezea maandalizi ya kilele cha Tamasha la Tuzo za Filamu Tanzania 2021.

“Kwa kuzingatia ukweli kwamba hizi ni Tuzo za kwanza za Serikali, hivyo Serikali haitakuwa sehemu ya kumnyima mtu haki ya ushindi kama kweli anastahili kushinda pasipo kutazama jina au umaarufu wa mtu, hata Wasanii wachanga wana haki ya kushinda Tuzo hizi”-Amesema Waziri Bashungwa.

Waziri Bashungwa ameeleza kuwa Serikali imeanzisha Tuzo hizo kwa mara ya kwanza kwa lengo la kutambua mchango wa Wanatasnia ya Filamu nchini ambapo kilele kitafanyika Desemaba18, 2021jijini Mbeya katika ukumbi wa Tughimbe.

Akielezea sababu ya kilele cha Tuzo hizo kufanyika jijini Mbeya amesama ni kutambua uwepo wa Wanatasnia ya Filamu pamoja na Wasanii wengine kwa ujumla wake Jijini humo, pamoja na kufungua milango ya fursa mbalimbali zilizoko Mbeya ikiwemo kutumia Tuzo hizo kuonesha vivutio mbalimbali vya Utalii vinavyopatikana jijini humo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera amesema kupitia tuzo hizo ni fursa ya kipekee kwa wadau wa maendeleo kutembelea Mkoa wa Mbeya kujionea uzuri wake na kuwekeza katika sekta mbalimbali.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.