Star Tv

Waziri wa Utamaduni, Sana na Michezo Innocent Bashungwa ameonya tabia ya mashabiki wa timu kubeza timu zao pindi zinaposhindwa kufikia malengo au hatua iliyotamaniwa na mashabiki husika akisema kitendo hicho siyo cha kizalendo na kinawavunja moyo wachezaji.

Waziri Bashungwa ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wakazi wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, katika kilele cha mashindano ya mpira wa miguu wa jimbo la Korogwe yaliyopewa jina la Dkt. Kimea Cup

Waziri Bashungwa amesema Watanzania hawana budi kutambua kuwa michezo mingi humalizika kwa matokeo ya aina tatu, ambayo ni kufunga, kufungwa na kutoa sare, hivyo mashabiki hawana budi kuwa tayari kuyapokea matokeo yote matatu.

“Nyinyi nyote mnaoshindana leo ni wazuri ndiyo maana mmefikia fainali, hivyo nyote ni wangu lakini lazima mjue kwamba kwenye mchezo wa mpira wa miguu kuna kushinda, kushindwa na kupata sare, yote ni matokeo na yote lazima watanzania tuwe tayari kuyapokea”- alisema Waziri Bashungwa wakati akizungumza kabla ya mchezo baina ya timu mbili zilizoingia fainali katika mashindano hayo.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Korogwe Mjini Dkt. Alfred Kimea amesema mashindano hayo yameinua vipaji vya vijana wengi katika jimbo la Korogwe mji, ambavyo atahakikisha kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali wanaendeleza vipaji hivyo vya soka kwa manufaa ya vijana na jamii nzima ya Korogwe na Tanga kwa ujumla.

Mashindano ya Dkt. Kimea Cup yalishirikisha timu 12 kutoka kwenye kata 11 za Jimbo la Korogwe mji na kuziwezesha timu ya kata ya Kwamndolwa na kata ya Mgombezi kuingia katika fainali ya mashindano hayo, mchezo uliochezwa katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Korogwe (Korogwe TCC) Novemba 21, 2021.

Latest News

MATETEMEKO MAWILI YA ARDHI YAUA WATU 22 AFGHANISTAN.
18 Jan 2022 09:36 - Grace Melleor

Takriban watu 22 wafariki kufikia sasa baada ya matetemeko ya ardhi ya mfululizo kukumba magharibi mwa Afghanistan siku  [ ... ]

WAZIRI MKUU AWATAKA MABALOZI KUVUTIA WAWEKEZAJI.
17 Jan 2022 16:24 - Grace Melleor

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika mataifa mbalimbali watoe msukumo Katika u [ ... ]

RAIS WA MALI ALIYEPENDULIWA MADARAKANI AFARIKI.
17 Jan 2022 06:53 - Grace Melleor

Rais wa Mali aliyeondolewa madarakani Ibrahim Boubacr Keita amefariki akiwa na umri wa miaka 76, familia yake na rafiki  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.