Star Tv

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kukamilisha andiko ili kuzuia matumizi ya kamba za plastiki.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo wakati alipotembelea kiwanda hicho ambacho kabla ya kufanyiwa maboresho kilikuwa kinazalisha tani 1.5 hadi 2.5 kwa siku ambapo kwa sasa kinazalisha tani 20 kwa siku.

"Leo tunalima mkonge, hapa Tanga mnalima mkonge na zinazalisha kamba za katani, kamba Tanzania ni nyingi, likishatoka tangazo hakutakuwa na ruhusa ya kutumia kamba za plastiki nchini"

Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba atoe kipaumbele wakazi wa eneo la Ngomeni katika suala la ajira kwenye kiwanda cha kuzalisha bidhaa zinazotokana na zao la mkonge cha Sisalana.

NSSF ilitoa takribani shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya kukifufua ikiwa ni utekezaji wa kampeni ya ujenzi wa viwanda katika kiwanda hicho kilichoko katika eneo la Ngomeni Mkoani Tanga ambacho

Waziri Majaliwa amesema kwa kuwa kiwanda hicho ambacho kipo katika kata ya Ngomeni wilayani Muheza ni vema kwa uongozi wa NSSF ukatoa kipaumbele cha ajira kwa wananchi wanaozunguka eneo ili waweze kunufaika na uwepo wake.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amewaagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF pamoja na Afisa Kazi wa Mkoa wa Tanga wakutane na waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda hicho na kushirikiana nao kutatua changamoto zinazowakabili.

Kampuni ya Sisalana ilianza kazi rasmi kiwandani Machi 12, 2021 ambapo ilikuta hali ya uzalishaji ikiwa ni ya kusuasua kutokana na ukosefu wa mtaji wa kuendeshea biashara na uchakavu wa mitambo.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.