Star Tv

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea mazoezi ya timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Tanzania (Taifa Stars) na amewaeleza wachezaji kwamba Watanzania wanamatarajio makubwa kwamba timu yao itafuzu na kushiriki kombe la Dunia litakalofanyika, Qatar 2022.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wachezaji wa Timu hiyo katika uwanja wa Benjamin William Mkapa jijini Dar es Salaam baada ya kushuhudia mazoezi ya timu 

“Nimekuja kuona mwenendo wa mazoezi, matarajio tuliyonayo ni makubwa na tuna imani mtashinda. Mechi ya keshokutwa ni muhimu kwa nchi yetu tunahitaji kushinda mechi zilizobaki ili tutimize malengo yetu. Tunahitaji kuweka historia.”-Majaliwa.

Taifa Stars inafanya mazoezi ya kuajiandaa na michezo ya awali ya kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Timu ya Taifa ya DR Congo na Madagascar, ambapo Majaliwa amewasisitiza wachezaji wazingatie mafunzo yanayotolewa na walimu.

Waziri Mkuu amesema Serikali kupitia Wizara ya Michezo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wataendelea kuisimamia na kufuatilia maendeleo ya timu hiyo hadi hatua ya mwisho na kuhakikisha inafanya vizuri.

Kwa upande wake, Nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta ambaye amezungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake amesema wamejiandaa vizuri na kwamba watahakikisha wanapata ushindi katika mechi zote zilizobaki.“Tutapambana kwa ajili ya nchi yetu.”

Latest News

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Urusi Kuchagiza Maendeleo Afrika kupitia Nishati ya Nuklia na Madini ya Urani
12 Aug 2023 10:07 - Kisali Shombe

ROSATOM, taasisi ya nishati ya nyuklia ya serikali ya Urusi ambayo iliwaalika zaidi ya waandishi wa habari 15 kutoka nch [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.