Star Tv

Serikali imetoa wito kwa wasanii kuendelea kusajili kazi zao katika mamlaka zinazo husika ili zilindwe kisheria na mamlaka hizo katika kuhakikisha zinawanufaisha na kufanikisha ndoto zao.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa wakati akijibu maswali ya baadhi ya Wabunge waliotaka kujua msimamo wa Serikali katika kuthibiti wizi wa kazi za Sanaa kupitia ombwe kubwa la uwepo wa teknolojia zinazo wawezesha wezi kudurufu kazi za wasanii na kuziuza bila kibali cha msanii husika.

Katika kikao hicho baina ya watendaji wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma, na Maendeleo ya Jamii, Waziri Bashungwa amewaelezea wajumbe kuwa nia ya Serikali ni kuona vijana wananufaika kupitia kazi zao, lakini kwa kufuata Sheria za nchi, Kanuni, Taratibu na Miongozo iliyowekwa kwa lengo la kulinda maslahi yao.

“Kwa hiyo ndugu zangu wajumbe tuendelee kusaidizana kuwahimiza hawa vijana wetu kila mmoja kwa nafasi yake kwamba ni muhimu kusajili kazi zao, ili linapotokea suala la kuibiwa kazi tuwe na meno na sehemu ya kuanzia kisheria katika kufuatilia haki ya msanii husika”- Amesema Waziri Basungwa mbele ya kamati hiyo ya Bunge.

Awali Katibu Mkuu wa Wizira ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema Wizara hiyo inaendelea na uratibu kuona namna bora inavyoweza kuwapeleka wataalamu wa sanaa nje ya nchi kujifunza na kuongeza ujuzi zaidi ili baadae warejee hapa nchini kuwasaidia wasanii na hasa wasanii wachanga kuzalisha kazi zenye ubora zaidi.

Akizungumza kabla ya kuahirisha kikao hicho, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma, na Maendeleo ya Jamii, Aloyce Kamamba amepongeza hatua zinazofanywa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ikiwa ni pamoja na hatua ya kuwezesha kutengwa kwa asilimia tano ya mapato kutoka kwenye michezo ya kubahatisha ambayo inaiwezesha Wizara kupata fedha kiasi cha shilingi Milioni 400 kwa kila robo ya mwaka kutokana na asilimia hiyo.

Latest News

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Urusi Kuchagiza Maendeleo Afrika kupitia Nishati ya Nuklia na Madini ya Urani
12 Aug 2023 10:07 - Kisali Shombe

ROSATOM, taasisi ya nishati ya nyuklia ya serikali ya Urusi ambayo iliwaalika zaidi ya waandishi wa habari 15 kutoka nch [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.