Star Tv

Waziri wa Biashara na uchumi nchini Ufaransa Franck Riester amezindua magari ya umeme yaliyoundwa na kampuni ya E-Motion Africa hapa nchini.

Kampuni ya E-Motion Africa iliundwa mnamo 2019 kwa lengo la kutoa suluhisho la asili na rahisi kwa changamoto ya usafiri unaotoa gesi ya kaboni hapa nchini na inapendekeza kubadilisha injini ya dizeli ya magari ya uchukuzi kuwa magari ya umeme, unayotumia na nguvu ya betri.

Kwa mujibu wa gazeti la The Citizen Waziri Riester amenukuliwa akisema “Gari lisilotoa gesi chafu ndio gari la siku zijazo”.

Riester amesema Ufaransa imejitolea kukuza ushirikiano na kushirikiana kiteknolojia na Tanzania.

Mradi huo ulianzishwa na kampuni ya safari ya Ufaransa Mount Kilimanjaro Safari Club (MKSC) ambayo imekuwa ikifanya kazi kwa miaka 20 Kaskazini mwa nchi katika mbuga za kitaifa.

#ChanzoTheCitizenNaBBCSwahili

Latest News

SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA WATU NANE SOMALIA.
25 Nov 2021 10:26 - Grace Melleor

Polisi nchini Somalia wamethibitisha vifo vya raia katika bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji mkuu Mogadishu, tele [ ... ]

WAZIRI MKUU SWEDEN AJIUZULU SAA CHACHE BAADA YA KUTEULIWA.
25 Nov 2021 09:01 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke kuwahi kushikilia wadhifa huo nchini Sweden amejiuzulu saa chache mara baada ya kuteuliwa [ ... ]

MTOTO WA GADDAFI AZUIWA KUGOMBEA URAIS LIBYA.
25 Nov 2021 07:13 - Grace Melleor

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania uchaguzi wa  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.