Star Tv

Jumla ya wakala wa forodha 50 wanaotarajiwa kutoa mafunzo kwa mawakala wa forodha visiwani Zanzibar wamekabidhiwa vyeti vya kiwango cha Afrika mashariki cha utoaji wa huduma za uwakala mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo yaliotolewa na wataalamu wa ITA.

Mafunzo hayo yalilenga kupunguza au kuondoa makosa mbalimbali yanayofanywa na mawakala wa forodha na kuikosesha mapato Serikali.

Kukamilika kwa mafunzo hayo kutasaidia mamlaka ya ya kodi Tanzania TRA kufikia malengo yanayopangwa na serikali katika ukusanyaji kodi kupitia vianzio vya bandari na viwanja vya ndege hali inayotegemewa kuoengeza mapato na kuiwezesha serikali iweze kutoa huduma bora kwa wananchi.

Wakati akifungua mafunzo hayo rais wa taasisi ya wakala wa forodha Zanzibar ZFB Omar Husein anasema kutokana na kukamilika kwa mafunzo hayo ya kwanza visiwani hapa watatanua wigo wa kuendesha huduma kwa ufanisi zaidi.

Msimamizi wa mafunzo hayo kutoka mwamvuli wa vyama vya mawakala wa forodha Afrika mashariki yenye makao yake nchini Kenya Elias Baluku anasema anatarajia mabadiliko na kutokufanya kazi kwa mazoea.

Baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo ya cheti cha kiwango cha Afrika Mashariki kwa utoaji wa huduma ya uwakala wa forodha wanaelezea mabadiliko wanayotegemea kwa mawakala ambao watawafikishia mafunzo walioyapata.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.