Star Tv

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi zinachangia katika kuinua uchumi wa Watanzania.

Waziri Mkuu amesema hayo leo Septemba 22, 2021 baada ya kuzindua Maonesho ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini mkoani Geita.

Waziri Majaliwa amesema maonesho hayo yamekuwa na manufaa makubwa katika kuhamasisha wananchi kujihusisha na shughuli za madini.

"Mheshimiwa Rais, anawaahidi kuendelea kuchukua hatua madhubuti katika kulinda na kuendeleza rasilimali hizi ili ziweze kuwanufaisha na kuwaletea maendeleo Watanzania wote, tuendelee kuunga mkono."

Amesema Serikali itaendelea kufanya marekebisho ya baadhi ya kanuni na taratibu zinazosimamia uchimbaji na biashara ya madini kwa lengo la kuwezesha wananchi na wadau mbalimbali kushiriki ipasavyo katika uchumi wa madini na kuongeza uwekezaji.

Hata hivyo, Waziri Majaliwa amewataka wadau wa sekta ya madini nchini wazingatie na wafuate sheria, kanuni, taratibu na miongozo inayosimamia sekta hiyo ili kuondoa usumbufu na kurahisisha utendaji wa shughuli zao na Serikali kwa manufaa ya pande zote.

Amesema sekta ya madini imeendelea kutoa mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa na maendeleo ya mtu mmoja mmoja nchini. “Matarajio ya Serikali ni kuongeza zaidi mchango huo kupitia shughuli za uchimbaji, uchenjuaji, usafishaji madini, usanifu madini na utoaji wa huduma katika shughuli za madini.”

Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kuweka mikakati ya kuimarisha Taasisi ya Jiolojia Tanzania (GST) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ili ziweze kutoa huduma bora na nafuu kwa wachimbaji wadogo ikiwa ni pamoja na uchorongaji wa miamba ili kujua uwepo na wingi wa mashapo.

Kwa upange wake, Waziri wa Madini Dotto Biteko amesema Wizara ya Madini itaendelea kusimamia biashara ya madini nchini ili kuhakikisha ndoto ya Rais Mheshimiwa Samia ya kutaka kuona Tanzania inakuwa kitovu kikubwa cha biashara ya madini inatimia.

Aidha, Rais wa Muungano wa Wachimbaji Wadogo Tanzania, John Mbina ameipongeza Serikali kwa namna inavyosimamia ukuaji wa sekta ya madini nchini.

Awali, Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha kusafisha madini ya dhahabu cha Geita Gold Refinery (GGR) kinachomilikiwa na Mtanzania kilichopo eneo la Bombambili ambapo amesema kuwa Serikali itafanya jitihada ili kuhakikisha kiwanda hicho kinafanya kazi kama ilivyokusudiwa.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.