Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amewapongeza vijana wa Timu ya Taifa Stars na Watanzania wote kwa ushindi wa Magoli 3 - 2 dhidi ya Timu ya Madagascar kwenye mchezo uliochezwa leo Septemba 07, 2021 wa Michuano ya kufuzu kombe la Dunia 2021.
Bashungwa ameeleza kuwa Wizara itawapa zawadi ya Tsh 10,000,000 kuwapongeza kwa jitihada safi ya mapambano ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia mwaka 2021.
Ushindi huo unaifanya Stars kuwa kileleni katika msimamo wa kundi J ikiwa na alama 4.
Mabao ya Stars yamefungwa na
- Erasto Nyoni-Penalti
- Novatus Dismasi
- Feisali Salum Abdallah
Aidha, Bashungwa ametoa wito kwa kuwaomba wadau wowote mwenye zawadi kwa Taifa Stars wawasiliane na Wizara ili kutambua zawadi ya michango hiyo ya hamasa kwa Taifa Stars.