Star Tv

Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema tozo za miamala ya simu si michango ya kirafiki ni sheria iliyopitishwa na Bunge baada ya kujadiliwa kwa kina akibainisha kuwa wabunge ni wawakilishi wa wananchi.

Dkt.Nchemba amezungumza hayo leo Ijumaa Agosti 20, 2021 katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

“Yaani inanyesha mvua moja tu mtoto inabidi alale shuleni hivi nani anaweza kumuamini jirani tu mtoto alale kila siku......niambie mzazi unalala usingizi wa aina gani, kuna vitu ni serious kweli kweli ambavyo wabunge wanavisemea ambavyo vinatulazimisha tufunge mikanda"- Dkt Mwigulu.

Aidha, waziri Mwigulu amesema kuwa fedha zilizopatikana baada ya ukusanyaji wa tozo tangu sheria ilipoanza kutumika mwezi mmoja uliopita, zimetumika kuboresha sekta ya afya, elimu na miundombinu.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.