Star Tv

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP. Simon Sirro, amewataka Wananchi na Watanzania kwa ujumla wasidanganywe na watu wachache au kikundi cha watu wanaowahamasisha kwa njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii kutokuchanjwa chanjo ya Uviko-19 (COVID-19).


IGP. Sirro ametoa kauli hiyo ikiwa imepita siku moja mara baada ya zoezi la uchanjwaji wa chanjo hiyo kuzinduliwa hapo jana Julai 29, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Ikulu Dar es salaam.

“Niwaombe Watanzania wenzangu, niwaombe sana habari ya kupotosha suala la chanjo tusilipe nafasi, maisha hayaji huwa hayaji mara mbili, ukiondoka umeondoka wewe”- IGP. Simon Sirro.

Katika upande mwingine IGP. Sirro ameandikishina hati ya makubaliano kati ya Shirika la Bima la Taifa na Jeshi la Polisi kupitia Shirika lake la uzalishaji mali ambapo shirika hilo litaweza kuwa wakala wa bima za maisha na ajali kwa watendaji wa Jeshi hilo la Polisi pamoja na familia zao.

Kupitia bima hiyo Jeshi hilo limetoa ahadi ya kutanua wigo ili bima ya maisha iweze kuwafikia hata waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda, Ambapo amesema itasaidia kwakuwa ajali nyingi zilizopo hospitali ni za vijana wa bodaboda.

“Ndugu zangu kuwa na hii bima manake ni lazima, ukienda Muhimbili ukaingia mochwari wengi wao waliofariki ni kutokana na ajali ya bodaboda kwa kuwa biashara ile huwa haina tabu, unanunua pikipiki asubuhi unajifunza asubuhi jioni unaingia barabarani unaanza biashara ya boda boda na unakuta wana familia hivyo wanapofariki wanaziacha zinataabika, lakini kupitia hii bima itasaidia kutoacha familia zao zikitaabika ikiwa itatokea wamepata ajali wakaaga dunia”-Alibainisha IGP. Sirro.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa Dkt. Elirehema Joshua amesema kuwa licha ya kuwepo kwa idadi ndogo ya wananchi wenye ufahamu wa masuala ya bima za maisha, ajali na mali ambapo kupitia shirika la uzalishajimali la Jeshi la Polisi litakuwa na wigo mpana wa kuwafikia wananchi pamoja na kuwezesha Watanzania wote kupata elimu na huduma zote za bima zinazopatikana nchini.

Latest News

KENYA YAPIGA MARUFUKU FILAMU YA WAPENZI WA JINSIA MOJA.
23 Sep 2021 14:44 - Grace Melleor

Bodi ya Filamu Kenya inasema kuwa filamu kuhusu maisha ya wanandoa wa jinsia nchini Kenya imepigwa marufuku nchini humo. [ ... ]

SHIL. MIL. 700 ZATOLEWA KUKARABATI BARABARA KARAGWE.
23 Sep 2021 13:55 - Grace Melleor

Serikali imetoa Shilingi Milioni 700 kusaidia ukarabati wa barabara za vijijini katika jimbo la Karagwe mkoani Kagera il [ ... ]

BABA AKAMATWA KWA KUCHOMA 'MATITI' YA BINTI YAKE.
22 Sep 2021 13:32 - Grace Melleor

Polisi katika jimbo la Nigeria la Lagos wamemtia nguvuni mwanaume mmoja kwa madai ya kuyaondoa matiti ya binti yake mwen [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.