Star Tv

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema John Mnyika amesema kamati kuu ya chama hicho itakaa Julai 22 mwaka huu ili kujadili ni maelekezo gani kama chama wanapaswa kutoa kwa wanachama ya kumtafuta mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, ambaye hajulikani alipo mpaka sasa.

Akizungumza na wanahabari Mnyika amesema kama chama hawafamu mwenyekiti wao Freeman Mbowe alipo na kuwaomba wananchi wasaidie kumtafuta

Mnyika amewaomba viongozi na wanachama wa Chadema nchi nzima wapaze sauti zao kumtafuta Mbowe.

“Ikiwa mpaka kufikia kesho Mwenyekiti wetu hatapatikana tutakwenda makamani”- Katibu Mkuu wa CHADEMA John mnyika.

Mbowe na wenzake 11, wamekamatwa ikiwa ni saa chache zilikuwa zimebaki kabla ya kufanyika kwa kingamano la kudai Katiba mpya, mkoani humo.

Kongamano la Kudai Katiba Mpya lililokuwa limepangwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kufanyika Jijini Mwanza limeshindikana mara baada ya viongozi Wakuu wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe kudaiwa kukamatwa usiku wa Manane wakiwa wamelala kwenye Hoteli Walizofikia.

Kongamano hilo lilipangwa kufanyika Jumatano hii Julai 21, 2021 jijini Mwanza ambalo lililenga kuwashirikisha viongozi na wanachama mbalimbali wa chama hicho wakiongozwa na mwenyekiti Freeman Mbowe.

Baadhi ya wakazi wa jijini wa Mwanza ambao walikuwa wakipita katika barabara ya Bwiru wameshuhudia vikosi vya askari Polisi wakiwa wametanda, AQMbapo walotoa mtazamo wao kuiona ni hali ya kutisha na ya kusikitisha katika suala la haki katika demokrasia.

Aidha, Jitihada zilizofanywa na mmoja wa mwandishi wetu katika kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ramadhan Ng’anzi kuzungumzia tukio hilo hazikufanikiwa.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.