Star Tv

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kuboresha miundombinu ya bandari ili kuvutia idadi kubwa ya watumiaji zikiwemo nchi za ukanda wa Maziwa Makuu.

Waziri Mkuu Majaliwa amebainisha hayo wakati alipokutana na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Leonard Chamuliro, Mkurugenzi wa Bandari, TASAC, TBS, TMDA, Kamishna wa Forodha pamoja na wadau mbalimbali wa masuala ya usafirishaji.

Amesema lengo la kikao hicho ni kufanya tathmini ya hatua zilizofikiwa katika uboreshwaji wa huduma mbalimbali bandarini zikiwemo za upakuaji wa mizigo.

Waziri Mkuu amesema Serikali imejipanga kununua vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuhakikisha kuwa mizigo yote inayopitia bandarini inapakuliwa katika kipindi cha muda mfupi.

Amesema bandari za Dar es Salaam, Mtwara na Tanga zimefanyiwa maboresho makubwa, hivyo amewasisitiza wadau wa sekta binafsi waendelee kuleta meli za kutosha.

Waziri Mkuu amesema mbali na maboresho yaliyofanyika katika bandari hizo, pia bandari za Kabwe, Kasanga nazo zimeboreshwa pamoja na ujenzi wa bandari ya Karema ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo na abiria katika nchi za Congo, Zambia na Burundi.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Chamuriho amesema kuwa ujenzi ndani ya bandari ya Dar es Salaama unaelekeka kukamilika.

“Gati zote saba tumezimaliza na sasa tunamalizia eneo la makontena katika gati namba sita na saba ambalo litakamilika mwezi Agosti, 2021, hii itasaidia kuongeza ufanisi ndani ya bandari”-Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Chamuliro.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Msanja Kadogosa amesema kuwa Shirika hilo limefanikiwa kukarabati mabehewa zaidi ya 200 ya mizigo ambayo yanaenda nchi za Burundi na Kongo.

Kadogosa ameongeza kuwa katika mwaka huu wa fedha, Serikali imelitengea Shirika hilo bajeti kwa ajili ya kukarabiti mabehewa 660 na kazi ya ukarabati itaanza muda wowote, pia vichwa vingine tisa vitakarabtiwa kwa ajili ya kutoa huduma ya usafirishaji wa mizigo.

Wadau wa sekta ya bandari wameipongeza Serikali kwa hatua mbalimbali inazochukua katika kuboresha sekta hiyo na wameshauri hatua zaidi zichukuliwe ili kuvutia zaidi watumiaji wa bandari nchini.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.