Star Tv

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu ametoa sababu ya kwanini taasisi za dini zinazotoa huduma katika sekta za afya na elimu zinatozwa na serikali, Ambapo amesema kuwa ni kwasababu baadhi zinafanya biashara na si kutoa huduma kama ilivyozoeleka.

Rais Samia amesema hayo kupitia mkutano mkuu wa 31 wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania CCT alioufungua ambao umedfanyika mkoani Morogoro.

Rais amebainisha kuwa wakati mwingine taasisi za dini hujenga shule au hospitali katika eneo ambali serikali imekwishajenga kituo cha afya.

“Hapa ndipo panapokuja lile suala linalolalamikiwa la ushindani wa huduma, taasisi ya dini ina hospitali yake hapo Serikali inajenga kituo cha afya hapo kwa kuona wananchi wakienda huku wanatoa pesa nyingi zaidi kuliko wakipata huduma serikalini”-Amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema lengo la Serikali ni kupunguza ugumu wa maisha kwa wananchi ambapo suluhisho lake ni kufanya kazi kwa uwazi na kuaminiana ili wanaotoza kodi wajue taasisi za dini hazifanyi kazi kibiashara.

“Hapa utaona wale wamekusanya jasho la watu wengine sisi tunaenda kutoza kodi, haya yote ni kwa sababu hatukuwa na uwazi, niombe sasa tufanye kazi kwa uwazi na kuaminiana”-Ameeleza Rais.

Katika upande mwingine Rais amevunja ukimya wa sababu ya bei ya mafuta kupanda nchini akisema ni mkakati wa Serikali kuongeza fedha kwa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) ili kuimarisha ujenzi wa barabara hizo.

“Nataka niwape taarifa kwamba tumeongeza fedha kidogo kwenye mafuta. Pengine mmesikia kelele za mafuta, lakini tumeongeza Sh100 katika kila lita ya mafuta ili tuweze kukusanya fedha zikatusaidie kujenga barabara za vijijini”- amesema Rais Samia.

Aidha Rais amefafanua kuwa fedha nyingi zimepotea katika ujenzi na ukarabati wa barabara ambazo zimekuwa zikiharibiwa na mvua.

Latest News

“MAISHA HAYAJI MARA MBILI, TUSIPOTOSHE KUHUSU CHANJO”-IGP. Simon Sirro.
29 Jul 2021 11:30 - Grace Melleor

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP. Simon Sirro, amewataka Wananchi na Watanzania kwa ujumla wasidanganywe na watu wacha [ ... ]

“MIMI NI MAMA, BIBI, MKE NA RAIS, SIWEZI KUJIWEKA KATIKA HATARI”-Rais Samia....
28 Jul 2021 10:26 - Grace Melleor

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepokea chanjo dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19, Ambayo ameizindua leo Julai 28, Katik [ ... ]

MSICHANA AUAWA KWA KUVAA JEANS.
28 Jul 2021 09:51 - Grace Melleor

Msichana mmoja aliyejulikana kwa jina la Neha Paswan, mwenye umri wa miaka 17, anadaiwa kupigwa hadi kufa na watu wa fam [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.