Star Tv

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania, (TANAPA), limefungua fursa kwa wawekezaji wa ndani ya Tanzania kutembelea vivutio vinavyopatikana katika hifadhi za kanda ya Magharibi kkwa lengo la kuwekeza katika huduma mbalimbali. Hii inatokana na idadi ndogo ya watalii wa ndani na nje wanaotembelea hifadhi za ukanda huo.

Ofisi za kanda ya Magharibi ambazo zinajumuisha hifadhi 10 ambazo ni, Serengeti, Kisiwa cha Saanane, Burigi- Chato, Kisiwa cha Rubondo, Mto Ugalla, Kigosi, Ibanda-Kyerwa, Rumanyika Karagwe, Gombe na Milima ya Mahale.

Ziara hii imeongozwa na Kamishna msaidizi Beatrice Kessy- msimamizi kitengo cha maendeleo ya Biashara, Utalii na masoko katika hifadhi za taifa kutoka makao makuu ya TANAPA. Ambapo wawekezaji hawa wamepata fursa za kutembelea hifadhi hizi na kujionea vivutio vilivyopo hifadhini. wakianzia hifadhi za Gombe na milima ya Mahale hifadhi maarufu kwa kuwa na sokwe wakubwa. Ziara hii ikiwa ya siku 10 wawekezaji hoa watatembelea hifadhi 7 kati ya kumi ambazo ni, Burigi- Chato, Kisiwa cha Rubondo, Mto Ugalla, Ibanda-Kyerwa, Rumanyika Karagwe, Gombe na Milima ya Mahale.

Latest News

“MAISHA HAYAJI MARA MBILI, TUSIPOTOSHE KUHUSU CHANJO”-IGP. Simon Sirro.
29 Jul 2021 11:30 - Grace Melleor

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP. Simon Sirro, amewataka Wananchi na Watanzania kwa ujumla wasidanganywe na watu wacha [ ... ]

“MIMI NI MAMA, BIBI, MKE NA RAIS, SIWEZI KUJIWEKA KATIKA HATARI”-Rais Samia....
28 Jul 2021 10:26 - Grace Melleor

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepokea chanjo dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19, Ambayo ameizindua leo Julai 28, Katik [ ... ]

MSICHANA AUAWA KWA KUVAA JEANS.
28 Jul 2021 09:51 - Grace Melleor

Msichana mmoja aliyejulikana kwa jina la Neha Paswan, mwenye umri wa miaka 17, anadaiwa kupigwa hadi kufa na watu wa fam [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.