Star Tv

Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na vyombo vya habari, ambapo amevitaka vyombo hivyo kuendelea kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa.

Rais Samia amebainisha hayo wakati akizungumza na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari jijini Dar es Salaam.

"Kwa ujumla kama tunavyofahamu vyombo vya habari mbali ya kutoa taarifa kwa umma vina mchango mkubwa kulinda umoja wa kitaifa,..... usalama wa nchi na kuchochea shughuli za maendeleo pia vinasaidia sana kufichua maovu kwenye jamii"- Rais Samia


Katika upande mwingine kuhusu suala la Corona Rais Samia amesema serikali itafanya chanjo ya hiyari ili kwenda sambamba na Dunia inavyokwenda.

“Nilipoingia madarakani nilitamani tushughulike na hili jambo kama linavyoshughulikiwa ulimwenguni, na kwahiyo nikataka kujua ukubwa wake na tunalo hili janga kiasi gani, nikaunda kamati ya waataalam.........nilishasema nitakaa na wenzangu Wanasiasa tuone tunakwenda na siasa zetu katika mustakabali mpana wa Taifa, Nchi yetu ina vitu vingi, Corona inatupiga, uchumi umeshuka tunaupandisha nimesema nakwenda kuifungua Nchi naomba nipeni muda halafu tutakwenda kwenye mengine”—Rais Samia

Rais Samia Suluhu Hassan ameshiriki mahojiano na Wahariri wa Vyombo vya Habari mbalimbali kuhusu siku 100 tangu kuingia kwake madarakani, ambayo yamefanyika ikulu jijini Dar es Salaam.

Latest News

“MAISHA HAYAJI MARA MBILI, TUSIPOTOSHE KUHUSU CHANJO”-IGP. Simon Sirro.
29 Jul 2021 11:30 - Grace Melleor

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP. Simon Sirro, amewataka Wananchi na Watanzania kwa ujumla wasidanganywe na watu wacha [ ... ]

“MIMI NI MAMA, BIBI, MKE NA RAIS, SIWEZI KUJIWEKA KATIKA HATARI”-Rais Samia....
28 Jul 2021 10:26 - Grace Melleor

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepokea chanjo dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19, Ambayo ameizindua leo Julai 28, Katik [ ... ]

MSICHANA AUAWA KWA KUVAA JEANS.
28 Jul 2021 09:51 - Grace Melleor

Msichana mmoja aliyejulikana kwa jina la Neha Paswan, mwenye umri wa miaka 17, anadaiwa kupigwa hadi kufa na watu wa fam [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.