Star Tv

Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi kwa kuendelea kulisimamia Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) ili kukuza na kujenga uchumi ambao utanufaisha Watanzania wote.

Akihutubia katika Hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa 12 wa Baraza hilo lenye kauli mbiu ya “Ufanisi wa Biashara na Uwekezaji katika Uchumi wa Kati Tanzania” uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais Samia amesema kuwa sekta binafsi ni muhimili mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi yeyote duniani, kwa hiyo kupitia Baraza hilo serikali itaendelea kuipa kipaumbele sekta binafsi.

“Ni ukweli usiopingika kwamba Sekta Binafsi ni muhimili mkubwa wa maendeleo na kuna usemi mwingine kuwa sekta binafsi ni injini ya kukuza uchumi, kwa hakika dunia ya leo hakuna taifa lolote duniani linaloweza kujinasua kiuchumi bila kufanya kazi bega kwa bega na sekta binafsi, Serikali itaendelea kutoa ushrikiano kwenu”- Amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia alisema kuwa TNBC ni jukwaa la kuwaleta wadau wa biashara ya uwekezaji pamoja na Serikali katika uelewa wa pamoja kuhusu masuala muhimu ya maboresho ya mazingira ya biashara hasa kwenye mabadiliko ya Sera, Sheria na Kanuni ambazo zitaleta fursa kubwa wafanyabiashara kwenye sekta zote.

Akibainisha mchango wa TNBC katika kukuza uchumi, Rais Samia alisema kuwa hilo ni Baraza na jukwaa kubwa ambalo kila mfanyabiashara anapata utaratibu wa biashara na uwekezaji ili kukuza mitaji na kuchangia uchumi wa taifa kwa kutoa kodi.

“Baraza hili limekuwa chachu ya kuboresha na kuanzisha Sera, Sheria, Kanuni na taratibu za biashara na uwekezaji nchini, tumejionea leo kulikuwa na mambo mengi ya mafanikio na changamoto ambazo zimetajwa hapa……ahadi yangu ni kuwa tunakwenda kuyaangalia kwa pamoja sisi na Sekta Binafsi”, Amesema Rais Samia.

Rais Samia ametumia Fursa hiyo kuwashukuru Watangulizi wake katika kufanikisha kuanzishwa kwa baraza hilo na kusimamiwa ambapo ameahidi kuwa baraza litaendelea kufanya kazi na kusimamia uboreshwaji wa mazingira ya biashara hasa kwa wafanyabiashara wanawake ili waweze kukuza uchumi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti Sekta Binafsi (TPSF) Bi. Angelina Ngalula amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuweka mazingira mazuri ya biashara kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa pamoja na wawekezaji.

“Naomba nikupongeze Mhe. Rais, kutokana na uamuzi wako ulioufanya katika kuboresha mazingira ya Biashara na kuipa kipaumbele sekta binafsi, kumekuwepo na ushirikiano mkubwa kati ya sekta binafsi na Serikali katika majadiliano”-alisema Bi. Ngalula.

Aidha, Bi. Ngalula amempongeza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa usimamizi madhubuti wa mazao ya kimkakati hususani mchikichi, alizeti na mazao mengine ambayo sekta binafsi inahusika kuwekeza.

Baraza hilo lilianzishwa na Serikali mwaka 2001 na sasa ni miaka 20 tangu kuanzishwa kwake, na linatumika kama jukwaa la majadiliano kati ya Serikali na Sekta Binafsi ili kutoa nafasi ya kila upande kutoa mawazo na kuboresha sera, sheria na kanuni katika sekta ya uwekezaji na biashara.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.