Star Tv

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania kuendelea kujitoa kulipa kodi ili kuwezesha upatikanaji fedha za uhakika ambazo zitakuwa ni chachu ya kutimiza miradi ya kimkakati.

Rais Samia ametoa agizo hilo katika hafla ya uwekwaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa, Standard George kipande cha Mwanza Hadi Isaka chenye urefu wa kilomita 341, shughuli iliyofanyika kijiji cha fela wilaya ya Misungwi.

Ziara ya Rais Samia suluhu Hassan imeendelea Mkoani Mwanza ikitazamwa kuwa ni yenye kuleta tija katika hatua ya ufunguzi wa Miradi ya Maendeleo, Ambapo katika ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha tano Rais Samia amemtaka mkandarasi wa mradi huo kuzingatia muda miezi 36 (miaka mitatu) aliopewa kuukamilisha ujenzi wa kipande hicho.

Rais Samia amepata wasaa wa kunena na wananchi akidhihirisha nia ya serikali yake katika kutekeleza miradi ya kimkakati, ambapo kubwa zaidi amewakata wananchi kulipa kodi ili dhamira ya kukamilisha miradi ya kimkakati iweze kutimia.

“Utekelezaji wa Reli pamoja na miradi mingine inahitaji fedha nyingi hivyo basi nawasihi sana Wanamwanza na Watanzania kwa ujumla kuendelea kulipa kodi, kodi hizo zinazolipwa ndizo serikali tunazokusanya na kutupa jeuri ya kufanya miradi ya aina hii”-Alisema Rais Samia.

Aidha katika hatua nyingine awali Rais Samia amezindua mradi wa maji ulioko katika mji wa Misungwi ambao umejengwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 13 ukiwa na uwezo wa uzalisha ujazo wa Milioni nne na nusu kwa siku.

Rais Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Maji kusimamia miradi ya maji ambayo haijakamilika ili kuwezesha wananchi kunufaika na miradi hiyo.

"Pamoja na jitihada tunayoiweka kuleta maji ndani ya mkoa wa Mwanza, wito wangu kwenu na ninaiagiza Wizara ya maji kuhakikisha miradi yote ambayo imebakia inakwenda kumalizwa na inatekelezwa kwa viwango vinavyotakiwa"-Rais Samia. 

Kutokana na kuzinduliwa kwa mradi huo ambao utawanufaisha wakazi 64,000 wa mji wa Misungwi na maeneo jirani Rais Samia amewataka wananchi kutunza miundombinu ya maji ili iwe endelevu kwa manufaa ya kizazi kilichopo na kijacho.

Mradi wa maji wa Misungwi na wa SGR imezinduliwa leo Juni 14, hii ikiwa ni siku ya pili ya ziara ya Rais Samia Mkoani Mwanza ambapo pia mapema asubuhi alikagua ujenzi unaoendelea katika Daraja la JPM (Kigongo-Busisi) ambalo litasaidia kurahisisha usafiri na usafirishaji pamoja na kukuza uchumi wa nchi na nchi za maziwa makuu.

Latest News

“MAISHA HAYAJI MARA MBILI, TUSIPOTOSHE KUHUSU CHANJO”-IGP. Simon Sirro.
29 Jul 2021 11:30 - Grace Melleor

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP. Simon Sirro, amewataka Wananchi na Watanzania kwa ujumla wasidanganywe na watu wacha [ ... ]

“MIMI NI MAMA, BIBI, MKE NA RAIS, SIWEZI KUJIWEKA KATIKA HATARI”-Rais Samia....
28 Jul 2021 10:26 - Grace Melleor

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepokea chanjo dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19, Ambayo ameizindua leo Julai 28, Katik [ ... ]

MSICHANA AUAWA KWA KUVAA JEANS.
28 Jul 2021 09:51 - Grace Melleor

Msichana mmoja aliyejulikana kwa jina la Neha Paswan, mwenye umri wa miaka 17, anadaiwa kupigwa hadi kufa na watu wa fam [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.