Star Tv

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 31 Mei, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Miradi wa taasisi ya The Susan Thompson Buffet Foundation Bi. Senait Fisseha ambayo inajihusisha na masuala ya afya ya wanawake.

Bi. Senait Fisseha amemueleza Mhe. Rais Samia kuwa taasisi hiyo ambayo imekuwepo hapa nchini kwa zaidi ya miaka 10 imetumia dola za Marekani takribani Milioni 90 (sawa na shilingi Bilioni 206) kufadhili miradi ya inayoshughulikia changamoto mbalimbali zinazohusiana na afya ya uzazi kwa wanawake na wasichana.

Amebainisha kuwa miradi hiyo imesaidia kukabiliana na vifo vinavyohusiana na ujauzito kwa kuwawezesha wanawake kupanga wakati gani wa kupata ujauzito, wakati gani wa kujifungua, kuepuka ujauzito katika umri mdogo na kujifungua salama.

Bi. Senait Fisseha ameshukuru kupata nafasi ya kuzungumza na Mhe. Rais Samia na amebainisha kuwa baada ya mazungumzo hayo taasisi hiyo ipo tayari kuendeleza miradi hiyo kwa kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Kwa upande wake, Mhe. Rais Samia ameishukuru taasisi hiyo kwa mchango wake katika masuala ya afya ya wanawake hapa nchini na amemhakikishia kuwa Serikali ya Tanzania ipo tayari kushirikiana nayo ili kukabiliana na changamoto zinawakabili wanawake na wasichana katika masuala ya afya.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichwale ambao baadaye wamefanya mazungumzo na Bi. Senait Fisseha kwa lengo la kujipanga namna taasisi hiyo itakavyofanya kazi na Serikali.

 CHANZO: IKULU 

 

Latest News

WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEA KULIPA KODI BILA KUCHOKA.
14 Jun 2021 19:01 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania kuendelea kujitoa kulipa kodi ili kuwez [ ... ]

WAZIRI MKUU MPYA AAPA KUIUNGANISHA ISRAEL.
14 Jun 2021 06:33 - Grace Melleor

Waziri Mkuu mpya wa Israel Naftali Bennett ameapa kuliunganisha taifa hilo ambalo linalezwa kufadhaishwa na chaguzi nne  [ ... ]

RAIS SAMIA AZINDUA KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU NA JENGO LA BOT.
13 Jun 2021 14:11 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua kiwanda cha kusafisha dhahabu jijini Mwanza kinach [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.