Mchezaji wa timu ya mpira wa miguu wa klabu ya Crystal Palace inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza (EPL) na Mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa amekubali ombi la Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuwa Balozi wa hiari wa utalii wa Tanzania.
Mamadou Sakho amekubali ombi hili wakati alipokutana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TTB, Betrita Lyimo katika Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro.
Mamadou ambaye ni raia wa Ufaransa amekuwa nchini kwa mapumziko ya siku 10 akiwa ameambatana na familia yake ambapo alitembelea maeneo ya utalii nchini yakiwemo Hifadhi ya wanyama ya Serengeti.
#ChanzoBBCSwahili