Star Tv

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kabla ya kupokea chanjo ya virusi vya Corona ni lazima serikali ijiridhishe kwanza juu ya chanjo hiyo ikiwa ni pamoja na kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa COVID-19.

Rais Samia amesema Ugonjwa wa Covid-19 umeathiri dunia nzima na ili kukabiliana nao lazima kushirikiana na mataifa mengine lakini Serikali itaendelea kuchukua tahadhari mbalimbali ikiwemo matumizi ya chanjo ya ugonjwa huo.

Rais ametoa kauli hiyo leo Mei 14, 2021 katika Baraza la Eid El-Fitir ambalo limefanyika muda wa jioni katika viwanja vya Karimjee mkoani Dar es Salaam.

“Nataka kuhakikishia kwamba tahadhari mlizitoa hapa juu ya chanjo na mengine zitafuatwa kikamilifu na Serikali yenu, hata hivyo hii haina maana kwamba tutapokea kila kitu tunacholetewa au kuambiwa la hasha lazima na sisi tujiridhishe kwa hiyo…tutajiridhisha kabla ya kuamua kutumia au kuacha kutumia, hivyo nawasihi Watanzania kutokuwa na hofu yoyote Serikali ipo makini sana katika kushughulikia suala hilo,” - Amesema Rais Samia.

Aidha, kwa upande wake Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir amewataka Waislamu kuzingatia maagizo yanayotolewa na wataalam wa afya kuhusu kujikinga na maambukizi ya magonjwa mbalimbali ukiwemo Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona.

“Kuna jambo limezungumzwa katika salamu zetu za baraza kuhusu afya. Afya ndio itakayotufanya tuweze kuswali, kufanya ibada, kushughulika masuala ya kiuchumi, kufanya biashara. Uislamu unasema kuilinda afya ni jambo la lazima, tufuate maelekezo ya wataalam wa afya kwa ajili ya kujikinga na magonjwa mbalimbali ikiwemo corona.”-Sheikh Abubakar Zubeir Mufti wa Tanzania

Waumini wa Dini ya Kiislam wameiadhimisha sikukuu hii ya Eid ambapo wametakiwa kuendelea kutenda matendo yaliyo mema kama ambavyo walikuwa wakitenda katika kipindi cha mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Latest News

WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEA KULIPA KODI BILA KUCHOKA.
14 Jun 2021 19:01 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania kuendelea kujitoa kulipa kodi ili kuwez [ ... ]

WAZIRI MKUU MPYA AAPA KUIUNGANISHA ISRAEL.
14 Jun 2021 06:33 - Grace Melleor

Waziri Mkuu mpya wa Israel Naftali Bennett ameapa kuliunganisha taifa hilo ambalo linalezwa kufadhaishwa na chaguzi nne  [ ... ]

RAIS SAMIA AZINDUA KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU NA JENGO LA BOT.
13 Jun 2021 14:11 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua kiwanda cha kusafisha dhahabu jijini Mwanza kinach [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.