Star Tv


Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania iko tayari kuwapokea wawekezaji kutoka Kenya pamoja na kuondoa vikwazo visivy vya kodi ambavyo vinaathiri biashara kati ya mataifa hayo mawili.

Rais Samia ametoa kauli hiyo wakati akiwahutubia wafanyibiashara kutoka Kenya na Tanzania, ambapo amesema hakuna nchi inayoweza kunawiri pekee yake bila ushirikiano na vikwazo vya kodi vilivyokuwepo.

Rais Samia amewatia moyo wafanyabiashara walioshiriki katika mkutano huo kwa kusema kwamba wawekezaji hawafai kushindwa kuwekeza katika mataifa hayo mawili;

"Mna bahati kwamba nchi zetu mbili upande mmoja kuna Uhuru wa kufanya biashara na..…upande mwingine kuna Suluhu ya kuondosha vikwazo vya biashara."-Amesema Rais Samia

Rais Samia ameongeza kwamba lengo lake ni kuhakikisha kwamba wawekezaji wa kigeni wanajenga imani ya kuwekeza nchini Tanzania na ili kurahisisha hilo serikali imeanzisha miradi mbali mbali ya kimkakati ikiwemo ya moiundombinu kama barabara, reli, na bandari ili kupunguza gharama ya kufanya biashara.

Rais Uhuru Kenyatta kwa upande wake amesema nchi zote mbili zitachukua hatua ya kuhakikisha kwamba makubaliano yote yaliyoafikiwa na mawaziri wa Biashara wa nchi zote yanatekelezwa.

Bwana Kenyatta ameongeza kwamba Mawaziri hao watakutana katika kipindi cha wiki nne zijazo ili kujadili kuondolewa kwa vikwazo visivyo vya kodi ambavyo vinaathiri biashara kati ya Kenya na Tanzania.

Rais Samia amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili nchini Kenya kwa kulihutubia bunge la nchini humo ambapo mapema asubuhi ya leo Mei 05 pia alifungua kongamano la wafanyabiashara baina ya nchi hizo lililofanyika jijini Nairobi.

Latest News

WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEA KULIPA KODI BILA KUCHOKA.
14 Jun 2021 19:01 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania kuendelea kujitoa kulipa kodi ili kuwez [ ... ]

WAZIRI MKUU MPYA AAPA KUIUNGANISHA ISRAEL.
14 Jun 2021 06:33 - Grace Melleor

Waziri Mkuu mpya wa Israel Naftali Bennett ameapa kuliunganisha taifa hilo ambalo linalezwa kufadhaishwa na chaguzi nne  [ ... ]

RAIS SAMIA AZINDUA KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU NA JENGO LA BOT.
13 Jun 2021 14:11 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua kiwanda cha kusafisha dhahabu jijini Mwanza kinach [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.