Star Tv

Mkurugenzi wa mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA) na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi anasema kuwa Kimbunga Jobo kwa sasa kipo kilomita 236 kutoka kisiwa Cha mafia Mkoa wa Pwani nchini Tanzania.

“Kimbuga hiki kwa sasa kipo kilomita 236 kutoka mashariki mwa kisiwa cha mafia, na kwa mwenendo huu kitaendelea kuja katika maeneo ya nchi yetu, mawingu yanaendelea kusogea.”

Dkt. Kijazi amesema kwamba kimbunga Jobo kinaweza kufikia katika ziwa victoria, kwani dalili za mawingu zimeanza kuonekana upande wa ziwa Victoria.

Aidha, amebainisha kuwa Kimbunga hiki kinatarajiwa kufika maeneo ya nchi kavu au mwambao wa pwani ya bahari nchini Tanzania, kuanzia tarehe 25. Na maeneo yatakayo athiriwa ni Lindi, Mtwara, Pwani,Dar es salaam Unguja na ziwa Victoria.

Kwa upande wa athari zitakazo tarajiwa Dkt. Kijazi amesisitiza kuwa watu wanaofanya shughuli katika bahari kama wavuvi wachukue tahadhari dhidi ya kimbunga hicho, lakini pia wakazi wa Maeneo ya pwani ya bahari, kwasababu kunatarajiwa kuwa na mvua pamoja na upepo mkali.

“Athari ambazo zinatarajiwa ni upepo mkali baharini pamoja na mawimbi makala, lakini pia kikitua nchi kavu upepo mkali utakuwepo nchi kavu, mara nyingi vimbunga kuambata na mvua kubwa, kwa hiyo mafuriko yanaweza kutokea “-amesema Dkt. Kijazi.

Kwa mujibu wa mashirika ya kimataifa ya utabiri wa hali ya hewa, kimbunga hicho kinatarajiwa kuwa kikubwa zaidi kuwahi kutua hapa nchini tangu mwaka 1952.

Utabiri ulionyesha kuwa kimbunga hicho kilipiata Ushelisheli Aprili tarehe 22 kikiwa na kasi ya kilomita 130 kwa saa na kinatazamiwa kutua Tanzania Aprili 24 au 25.

 

Latest News

“TUTAJIRIDHISHA KABLA YA KUKUBALI CHANJO YA CORONA”- Rais Samia.
14 May 2021 18:24 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kabla ya kupokea chanjo ya virusi vya Corona ni lazi [ ... ]

SOMALIA YATANGAZA KUREJESHA UHUSIANO NA KENYA.
06 May 2021 17:57 - Grace Melleor

Somalia imetangaza kuwa inarejesha mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani ya Kenya baada ya kusitisha mahusiano hayo m [ ... ]

KENYA NA TANZANIA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA.
05 May 2021 15:39 - Grace Melleor


Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania iko tayari kuwapokea wawekezaji kutoka Kenya pamoja na kuondoa vikwazo visivy  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.