Star Tv

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta uliowasilishwa kwake na Waziri wa Michezo, Utamaduni na Urithi wa nchi hiyo, Balozi Amina Mohamed.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu nchini Tanzania, Gerson Msigwa inasema pia kwamba Rais Samia amefanya mazungumzo na Balozi Amina kuhusu dhamira yaTanzania na Kenya kuendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano katika nyanja mbalimbali hususani kiuchumi na kijamii.

Rais Samia amemhakikishia Rais Kenyatta kwamba Serikali ya Tanzania ipo tayari kuendeleza mambo mazuri yaliyokuwa yakifanywa na Rais mtangulizi Hayati John Magufuli na kutatua changamoto kati ya nchi hizo mbili.

Taarifa hiyo imesema Rais Samia amewataka Mawaziri na wataalamu wa Tanzania na Kenya wanaounda Kamati ya ushirikiano wa pamoja ambao hawajakutana tangu mwaka 2016 kukutana mara moja ili kufanyia kazi masuala mbalimbali ya kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili .

Aidha, Rais Kenyatta amemwalika Rais Samia kufanya ziara nchini Kenya ili kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

 

Latest News

“TUTAJIRIDHISHA KABLA YA KUKUBALI CHANJO YA CORONA”- Rais Samia.
14 May 2021 18:24 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kabla ya kupokea chanjo ya virusi vya Corona ni lazi [ ... ]

SOMALIA YATANGAZA KUREJESHA UHUSIANO NA KENYA.
06 May 2021 17:57 - Grace Melleor

Somalia imetangaza kuwa inarejesha mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani ya Kenya baada ya kusitisha mahusiano hayo m [ ... ]

KENYA NA TANZANIA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA.
05 May 2021 15:39 - Grace Melleor


Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania iko tayari kuwapokea wawekezaji kutoka Kenya pamoja na kuondoa vikwazo visivy  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.