Star Tv

Rais Samia Suluhu Hassan amewakumbusha viongozi wa serikali wajibu wao kadiri ya Wizara zao leo Aprili 06,2021 wakati akiwaapisha Makatibu Wakuu pamoja na Manaibu Katibu.

Tamisemi: "Mkashugulikie elimu na afya za watanzania, Special priority kwa shule za wasichana mkasimamie"

Barabara: TARURA na TAMISEMI…"barabara za vijijini. Halmashauri zenye uwezo kama tarura wakipungukiwa na mkurugenzi unazo peleka hizo fedha ukajenge barabara".

Haki za wananchi: "shughulikieni kero za wananchi….kuanzia leo rais, makamu wa rais na waziri mkuu tukija kwa wananchi tukakuta wananchi wana bango la kero mkurugenzi, mkuu wa wilaya umekwenda..na sio mkawazuie kuandika..tukisikiaaa…mmekwenda".

Vibali vya kazi: "watendeeni haki wawekezaji. msilazimishe eti post hii lazima mtanzania, hizi ni pesa zake. Makampuni yanafungwa sio uongo…naomba mkalisimamie hilo".

Kifuatacho:"Wakuu wa mikoa na Wakurugenzi ili serikali ikamilike sisi tunahitaji wawekezaji....ubabe urasimu na rushwa tukasimamiane. MSIFUKUZEE WAWEKEZAJI kwa urasimu na mizengwe, tukarudishe imani ya wawekezaji, Mifumo ya makusanyo na matumizi ya fedha ikaangaliwe upya".

Miradi ya vipaumbele.

"Tuna miradi mikubwa miwili ya urithi na wanasema ukichezea urithi Mungu anakulaani. Naomba twende tukasimamie hii miradi ya kimkakati. Kumekua na ucheleweshwaji wa malipo bila sababu...mimi ninadhani kuchelewesha ni mradi wa watu".

Mkandarasi akileta certificate mlipeni

PMG kasimamie hili...Ninaposema NINAOMBA sio kwa UDHALILI...ni lugha tu ya "kimama" natumia.

Mambo ya nje: "Mama nenda karudishe mahusiano yetu na nchi za nje. Wanasema ukitaka kufika haraka nenda peke yako, ila ukitaka kufika mbali nenda na wenzio".

Jamhuri ya Muungano ni BARA na ZANZIBAR

Viwanda na Biashara: "Concept ya EPZ, iko wapi??...pacha Kitila na Mwambe naomba muwe serious kwenye EPZ".

Masoko: "Watu wanazalisha sana...masoko yako wapi? (nyinyi na wizara ya kilimo) mjibu hili swali".

Madini: "Najua tuna ubia na Barrick....najua kuna maswala hayajakaa vizuri....kodi na vingine...tusitunishiane misuli. Tukae pamoja tutatue..Makubaliano tuliyoingia yale ya nickel etc...nyoosheni watu wachimbe tupate pesa".

‘Negotiation Team’ malizeni hayo yaliyoko huko ili tuanze kazi mambo yaende.

Uchimbaji kwenye hifadhi: "Kijazi unajua kuna madini kwenye maeneo ya hifadhi...na uliweka misuli. mwekezaji anagonga mlango umefungwa....fungueni huo mlango. Simba na tembo hawali hayo. Tuangalie opportunity cost ya kupunguza eneo la hifadhi".

Mererani:"Tumeweka ukuta na majeshi na madini bado yanatoroshwa. Kitalu C kimewekwa akiba ila kimeanza kuvamiwa...NASEMA SITAKI KUONA MTU KWENYE KITALU C".

Ardhi: "Kuna migogoro miingi sana na imekuwa facilitated na nyie nyie maafisa ardhi. Mkarekebishe".

Maji: Hapa hakuna compromise jua lije au mvua inyeshe, maji lazima yapatikane kwa kiwango kinachohitajika. Si mijini au vijijini...maji yapatikane.

Elimu: Fanyeni tathmini ya manufaa ya elimu kwa mtanzania. Kuna baba pale anaitwa kishimba...akisema watu wanacheeeka ila mimi hua namsikiliza.

Afya: Pamoja na kazi nzuri zinasofanywa kwenye "gereji zetu za watu"...tuna kazi ya kuwapa incentives watumishi wetu wa afya wafanye vizuri zaidi

Bima ya afya kwa wote: Wataalamu malizeni mlete serikalini huku tuliamue...kama linatekelezeka tutekeleze kama halitekelezeki tujadili

COVID: Nakusudia kuunda kamati ya wataalamu, waliangalie kwa ukubwa wake watushauri tuamue.

Kilimo: nafurahi kelele za pembejeo zimepungua....ila kuna madudu hayo yanakuja....yanaitwaje kwereakwerea??..aaah nzigee...eeeh nzige

Ujenzi na Uchukuzi: Nyie ndo mmebeba miradi ya miundombinu...wakandarasi wana malalamiko fidia zinachelewa na malipo yanachelewa

Local content: ipo ila hakikisheni inakwenda kwa mtanzania...kwenye consultancy, makampuni ya nje yanaomba ila hawaji. wakishalipwa hawaji wanatuma local representative...pesa inaenda nje ushauri wa ziada tulotegemea hakuna

Airport ya msalato...tumeimba sana Msalato! Msalato! ila msala hautimii, sasa huu msala ukatimie.

Nishati: Uala la LNG linakaribiana na wimbo wetu wa taifa, Kalemani, hebu tufikie hatma. ….tujue tunajenga au hatujengi…..wale wasitucheleweshe.

Utalii: Ngorongoro inatoweka....tulikubaliana watu waishi na wanyama ila sasa watu wanazidi kuliko wanyama……..watu wasiendelee kuongezeka.

Utalii na Covid: Mtashiriki kwe ile Kamati ya wataalamu....kipindi hiki cha COVID TZ ndo tumepokea wataliii wengi zaidi kuliko nchi zingine ila je effect yake ni nini?

Mawasiliano teknologia ya habari: Mkonga wa taifa ulindwe, huduma za mawasiliano...kulizuka rabsha hapa maswala ya mabando mkalituliza...kalitatueni kabisa na lisijirudie.

Masha umemaliza WCF, nimekukabidhi NSSF mfuko wa private sector....naomba kasimamie vizuri...na uhakikishe private sector wote wanaingiza pesa za watanzania, PSSSF najua mna hali mbaya saaana NAJUA ila sijateua mtu pale, bado tuna kazi ya kufanya.

Bandari: Erick muda wangu ni miezi sita hapo bandari...nitaa-ssess alafu tutazungumza baadaye. Najua bandari pale kuna makundi mawili....kundi hili na lile wewe huna kundi...wewe walikutupa mwanza...nmekurudisha...nakupa MIEZI SITA

Wewe wa TASAC...kuna madudu yenu hapo unayajua.....nimekuinua ukarekebishe..wewe kijana mimi ni mama...sasa 'UKINIZINGUA TUTAZINGUANA'.

Aidha, Hayo yote yamesisitizwa na Rais Samia Suluhu Hassan wakati akiwaapisha Makatibu Wakuu pamoja na Manaibu katika ikulu ya Jijini Dar es Salaam.

 

Latest News

“MAISHA HAYAJI MARA MBILI, TUSIPOTOSHE KUHUSU CHANJO”-IGP. Simon Sirro.
29 Jul 2021 11:30 - Grace Melleor

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP. Simon Sirro, amewataka Wananchi na Watanzania kwa ujumla wasidanganywe na watu wacha [ ... ]

“MIMI NI MAMA, BIBI, MKE NA RAIS, SIWEZI KUJIWEKA KATIKA HATARI”-Rais Samia....
28 Jul 2021 10:26 - Grace Melleor

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepokea chanjo dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19, Ambayo ameizindua leo Julai 28, Katik [ ... ]

MSICHANA AUAWA KWA KUVAA JEANS.
28 Jul 2021 09:51 - Grace Melleor

Msichana mmoja aliyejulikana kwa jina la Neha Paswan, mwenye umri wa miaka 17, anadaiwa kupigwa hadi kufa na watu wa fam [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.