Dr Philip Mpango amekula kiapo leo kuwa makamu wa Rais wa Tanzania, Hafla ya kuapishwa kwa Mhe. Dkt. Mpango imefanyika Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma.
Sanjari na uapisho huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe; Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo katika baraza la mawaziri ili kuimarisha utendaji kazi huku akimteua kuwa mbunge aliyekuwa katibu mkuu Kiongozi Dr Bashiru Ally, mhe, Mbarok Mbarouk na mhe, Libelata Mulamula.
Mawaziri wengine waliobadilishiwa majukumu ni Dr Mwigulu Nchemba kuwa waziri wa Fedha, Mawaziri waliofanyiwa mabadiriko wanatarajiwa kuapishwa April Moja, Chamwino Ikulu.