Star Tv

Mwili wa hayati Rais Dkt. John Pombe Magufuli utazikwa katika makaburi ya familia huko wilayani Chato, mkoani Geita leo Machi 26,2021.

Maelfu ya Watanzania tayari wameanza kujitokeza katika uwanja wa Magufuli uliopo Chato ambapo misa ya ibada maalumu itafanyika kabla maziko.

Mazishi hayo yataongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi amehudhuri pia, lakini vilevile viongozi wengine wa serikali akiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, pamoja na wabunge wa viti maalum akiwemo Ester Matiko na Halima Mdee.

Hayati Rais Dkt. Magufuli ni rais wa kwanza nchini Tanzania kufariki akiwa madarakani na hatua ambayo imeifanya Tanzania kuongozwa na rais mwanamke kwa mara ya kwanza, Rais Samia Suluhu Hassan.

Hayati Rais Dkt. Magufuli alifariki kutokana na maradhi ya moyo wakati alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam Machi 17,2021.

Latest News

RAIS TSHISEKEDI ADHIBITI BARAZA LAKE JIPYA LA MAWAZIRI.
13 Apr 2021 18:22 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatatu alitangaza baraza jipya la Mawaziri katika hatua ambayo inaimar [ ... ]

MALIPO YA NDEGE MPYA TATU YAKAMILIKA.
13 Apr 2021 18:04 - Grace Melleor


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema tayari serikali imekamilisha malipo ya ununuzi wa ndege mpya tatu.

WASAFIRI KUTOKA KENYA KUINGIA KARANTINI KWANZA IRELAND.
12 Apr 2021 13:43 - Grace Melleor

Wasafiri wanaoelekea Ireland kutoka Kenya watalazimika kujitenga kwa wiki mbili baada ya kuwasili katika nchi hiyo ya ba [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.