Star Tv

Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania TEC limetoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari zaidi dhidi ya ugonjwa wa virusi vya corona.

Katibu wa TEC Padri Charles Kitima hii leo kupitia mkutano na wanahabari amesisitiza kuwa tishio la corona bado lipo nchini na ongezeko la vifo bado linaendelea kuripotiwa ikiwemo vya mapadre na watumishi wa afya wa Kanisa Katoliki.

''Ndani ya miezi iliyopita Mapadri 25 wamepoteza maisha kwa matatizo ya kupumua. Masisita na manesi zaidi ya 60, Vifo vinaendelea, tuchukue tahadhari."-Dkt. Padre Kitima.

Kwa mujibu wa Dkt. Kitima japo serikali kupitia Wizara ya Afya imetoa waraka wa kuwataka watu kuchukua tahadhari bado kuna changamoto kwa kuwa watu hawabanwi kisheria kuchukua tahadhari.

''Changamoto tuipatayo kwa kuwa serikali haijasisitiza tahadhari, watu bado wana mtazamo kuwa corona haipo au imeisha kama ilivyokuwa mwaka jana."

Aidha, Dkt. Kitima pia amesisitiza kutegemea sala pekee pasipo kufuata tahadhari zinazotolewa na Wizara ya Afya hakutaweza kuondoa tatizo hilo hapa nchini.

Latest News

RAIS TSHISEKEDI ADHIBITI BARAZA LAKE JIPYA LA MAWAZIRI.
13 Apr 2021 18:22 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatatu alitangaza baraza jipya la Mawaziri katika hatua ambayo inaimar [ ... ]

MALIPO YA NDEGE MPYA TATU YAKAMILIKA.
13 Apr 2021 18:04 - Grace Melleor


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema tayari serikali imekamilisha malipo ya ununuzi wa ndege mpya tatu.

WASAFIRI KUTOKA KENYA KUINGIA KARANTINI KWANZA IRELAND.
12 Apr 2021 13:43 - Grace Melleor

Wasafiri wanaoelekea Ireland kutoka Kenya watalazimika kujitenga kwa wiki mbili baada ya kuwasili katika nchi hiyo ya ba [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.