Star Tv

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amezikwa nyumbani kwake katika kijiji cha Mtambwe Nyali mkoa wa Kaskazini Pemba.

Mwili wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, uliagwa mapema leo asubuhi katika msikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam kabla ya kupelekwa Zanzibar kwa ajili ya mazishi.

Viongozi mbalimbali wa kitaifa walishiriki ibada hiyo akiwemo Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na Kiongozi wa ACT-Wazalendo Zitto Kabwe.

Baadhi ya wananchi pamoja na viongozi waliohudhuria ibada ya mazishi ya Maalim Seif Sharif wamesema kuwa wamesikitishwa sana na msiba wa kiongozi huyo.

Mamia ya wazanzibari walijitokeza katika Viwanja vya Mnazi Mmoja vilivyopo mjini Unguja ambapo ndipo mwili ulipokelewa kutoka jijini Dar es Salaam kwa ajili ya dua kabla ya kusafirishwa kwenda kijijini kwake Mtambwe.

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.