Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John William Kijazi amefariki dunia.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imeeleza kuwa Balozi Kijazi amefariki dunia Jumatano Februari 17, 2021 saa 3 usiku katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma alikokuwa akipatiwa matibabu.
Aidha, Taarifa hiyo ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu imebainisha kuwa taratibu za mazishi ya Marehemu Balozi John William Kijazi zitatolewa.