Mazishi ya Mwanasiasa maarufu nchini Dkt. Muhammed Seif Khatib yanatarijiwa kufanyika kesho Februari 16, saa nne asubuhi huko Mpenda Unguja.
Mwanasiasa huyo amefariki dunia leo Jumatatu, Februari 15,2021 asubuhi mjini Unguja.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Familia yake, Meneja Mkuu Zanzibar Media Corporation pamoja na Mkurugenzi wa maelezo visiwani Zanzibar Dkt.Juma Mohammed.
Aidha, katika taarifa ya kifo chake iliyotolewa na vyanzo husika hakuna iliyoeleza sababu ya kifo chake.
Ramadhan Sendah ambaye ni Meneja Mkuu wa Zanzibar Media Corporation alitoa taarifa ya kifo cha kiongozi huyo na kusema kuwa taratibu za mazishi zitatolewa na familia yake.
Assallam allaykum,
Uongozi wa Zanzibar Media Coporation Ltd unasikitika kutangaza kifo cha Mkurugenzi mtendaji wake Dr. Muhammed Seif Khatib kilichotokea hii leo asubuhi, taratibu za mazishi zitatolewa na familia yake baadae hii leo. Seif Khatib (70), amefariki dunia leo Februari 15, 2021 asubuhi mjini Unguja.
Amewahi kuhudumu serikalini kwa nafasi mbalimbali kama waziri wa muungano/habari pia amewahi kuhudumu kama Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, wakati huo akiwa mbunge wa Jimbo la uzini, hadi umauti unamkuta alikuwa akimiliki vyombo vya habari vya Zenj fm/Zenj TV pamoja na gazeti la Nipe habari
Ramadhan Sendah
Meneja mkuu.
Dokta Khatib aliwahi kuwa mbunge wa jimbo la Uzini, Unguja na pia amewahi kuhudumu katika nafasi mbalimbali za uongozi wa chama tawala CCM.
Miongoni mwa nyadhifa nyingine, hadi anapatwa na mauti, alikuwa ni mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA).