Star Tv

Mkuu wa Wilaya ya Mjini visiwani Zanzibar, Rashid Msaraka ametangaza kuanza operesheni ya kuwanyoa nywele vijana wenye umri chini ya miaka 18, waliofuga rasta au kunyoa mtindo wa panki.

Bwana Rashid amesema kama vijana hao wanataka kufuga rasta hizo wakafugie sehemu nyingine na endapo wazazi wao wameshindwa kuwakata hizo nywele, atawakata yeye.

''Vijana wote wenye umri chini ya miaka 18 kama huyu..kama wazee wao wameshindwa kuwakata hizi nywele tutawakata sisi'' alitahadharisha kiongozi huyo.

Aidha, picha ya video imesambaa katika mitandao ya kijamii ikionesha msaidizi wa kiongozi huyo akimkata nywele kijana aliyekuwa amezisokota nywele zake.

Kitendo hicho kimeibua mjadala kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, watu wakihoji ni sheria ipi iliyomuongoza kiongozi huyo kutoa agizo la kumkata nywele kijana huyo.

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.