Star Tv

Kampuni nne za kitanzania zimeshinda zabuni yenye thamani ya shilingi Bilioni 7.5 kwa ajili ya ujenzi wa mkongo wa taifa pamoja na maboresho ya anwani ya makazi.

Ujenzi huo wa mkongo wa taifa utakuwa ni wa kilomita 409 ambapo utafikisha mawasiliano katika nchi Jirani ya Msumbiji pamoja na kuunganisha mawasiliano katika mikoa mingine ya Tanzania ikiwemo Singida na Mbeya.

Mikataba hiyo pia ni pamoja na maboresho ya anwani za makazi.

Wakati huo huo, Waziri Ndugulile ametilia mkazo suala la ubora na kuzitaka kampuni hizo kukamilisha kazi kwa wakati uliopangwa.

Akizungumza kwa niaba ya makampuni mengine yaliyosaini mikataba hiyo, ameihakikishia serikali kwamba watakamilisha kazi hiyo kwa wakati na ufanisi.

Hii ni mara ya kwanza kwa kampuni za ndani kushinda zabuni ya Ujenzi wa mkongo wa taifa, Ambapo tayari Tanzania imejenga wastani wa kilomita 7910 ya mkongo wa taifa kwa lengo la kurahisisha Mawasiliano na kufikia malengo ya uchumi wa kidigitali na biashara Mtandao.

Chanzo na BBC Swahili

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.