Star Tv

Chama cha ACT Wazalendo kimewafahamisha wanachama wake, pamoja na umma wa Watanzania kuwa Mwenyekiti wake Maalim Sei Sharif Hamad na mkewe Bi Awena, wamethibitika kupata maambukizi ya Covid 19.

Kulingana na taarifa ya chama iliyotumwa kwenye mitandao yake ya kijamii, ACT Wazalendo imesema kuwa wasaidizi kadhaa wa Makamu huyo wa Rais wa Zanzibar pia wamepatikana na virusi vya corona baada ya kufanyiwa vipimo.

''Katika hali ya kuchukua tahadhari zaidi madaktari walimshauri Maalim Seif kuwa ni vyema awepo chini ya uangalizi maalum katika kipindi chote atakachokuwa anaendelea na matibabu'', imesema taarifa ya ACT iliyotumwa kwenye ukurasa rasmi wa Twitter wa chama.

Kulingana na taarifa hiyo Maalim Seif amepumzishwa katika Hospitali ya Mzazi Mmoja, Unguja, ambako anaendelea kuwa chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari.

 

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.