Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli ameiomba serikali ya China kuisamehe Tanzania madeni ambayo Tanzania ilikuwa imekopa kutoka taifa hilo.
Moja ya deni ni Milioni 15.7 za kitanzania ambazo zilitumika wakati reli ya Tazara ikiwa inajengwa.
Deni lingine ni la fedha zilizotolewa wakati Tanzania inajenga nyumba za askari ambapo tayari Tanzania imerudisha zaidi ya nusu ya deni hilo na lingine ni ujenzi wa kiwanda cha urafiki kinadaiwa dola 15.
Rais Magufuli amesema, ameiomba China kuifutia Tanzania madeni kwa sababu China ni nchi rafiki kwa Tanzania na ni nchi tajiri.