Star Tv

Wakazi wanaoishi pembezoni mwa Mto Rau katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro wameingiwa hofu baada ya maji ya mto huo kugeuka kuwa rangi nyeusi.

Mto Rau ni Moja ya Mto ambao hutiririsha Maji yake kutoka kwenye Kilele cha Mlima Kilimanjaro na kumwaga maji yake kwenye Bonde la Pangani.

Mto huu sasa umewashangaza wengi hususani wakazi wanaoishi kuzunguka Mto huo, baada ya maji yake kuwa meusi kiasi cha kutishia usalama wa maisha ya wakazi wanaotumia maji hayo kwa shughuli mbalimbali za kijamii na kibadamu.

Mapambazuko na Machweo ya siku ,sasa yamegeuka kuwa gumzo kwa wakazi wa eneo hilo, ambapo hakuna mwenye majibu sahihi ya ukweli wa maji hayo kugeuka rangi na kuwa nyeusi.

Baadhi ya wakazi hao wameiomba serikali kuchunguza na kubaini chanzo kilichosasababisha Maji hayo kuwa na rangi nyeusi.

“Mimi nimekuja asubuhi hapa, nilikuwa nataka nioge nikakuta maji ni meusi, naiomba serikali itusaidie kuwa ni nini kimetokea”-Alisema Ayubu Mrutu, Mkazi wa Moshi

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt.Anna Mghwira naye amewaagiza wataalamu wake kuanza kuchunguza mara moja ili kubaini chanzo cha Maji hayo kugeuka kuwa na rangi nyeusi.

“Aaah! Ni maajabu kidogo lakini nimeagiza kitengo chetu cha maji kwa kushirikiana na wataalamu wa maji wawaalike wataalamu wengine wa maji, tuihusishe Wizara, tusaidiane kama kuna sababu za kisayansi tujue, kama kuna sababu zozote za kitamaduni tujue labda imewahi kutoke. Mambo haya kuna wakati mwingine lazima yaliwahi kutokea huko nyuma”-Bi.Anna Mgwhira, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Kiu ya wakazi wa eneo hilo ni kuona wanapata majibu sahihi juu ya chanzo cha maji hayo kuwa na rangi nyeusi, lakini hili ni swala la kusubiri na kuona sababu iliyopelekea maji hayo kuwa na rangi nyeusibaada ya wataalamu kulifanyia ufumbuzi kama alivyoagiza Mkuu wa Mkoa Bi. Mghwira.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.