Star Tv

Jumla ya wanafunzi 759,706 sawa na asilimia 91.1 ya wanafunzi waliofaulu wakiwemo wavulana 368,174 na wasichana 391,532 wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwaka 2021.

Kauli hiyo imebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo wakati akitoa taarfa ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwaka 2021 leo jijini Dodoma.

Akizungumza Mhe. Jafo amesema kuwa kati ya wanafunzi 4,169 wamechaguliwa kujiunga na shule za bweni ambapo wanafunzi 970 watajiunga na shule za wanafunzi wenye ufaulu mzuri Zaidi.

Pia Mhe. Jafo amesema kuwa wanafunzi 1,238 watajiunga na shule za ufundi, wanafunzi 1,961 watajiunga na shule za bweni za kawaida.

Wanafunzi 755,537 wakiwemo wavulana 362,247 na wasichana 385,665 wamechaguliwa kujiunga na shule za Sekondari za kutwa katika maeneo mbalimbali nchini.

“Miongoni mwa waliochaguliwa, wanafunzi wenye mahitaji maalum ni 2,491 wakiwemo wavulana 1,312 na wasichana 1,179 sawa na asilimia 75.0 ya wanafunzi wenye ulemavu waliofanya mtihani huo"-Waziri Jaffo.

Jumla ya wanafunzi 74,166 sawa na asilimia 8.9 wakiwemo wavulana 34,861 na wasichana 39,305 hawakupangiwa shule katika awamu ya kwanza kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.

“Hivyo wanafunzi wenye sifa ambao hawakupangiwa shule katika awamu hii ya kwanza watapangiwa shule katika awamu ya pili kabla ya tarehe 28 Februari, 2021”- ameeleza Mhe. Jaffo

Waziri Jafo amesema kuwa wanafunzi hao wataendelea kupangiwa shule kadri Mikoa na Halmashauri zitakavyoendelea kukamilisha vyumba vya madarasa na madawati hadi kufikia tarehe 28 Februari, 2021.

Aidha, amewaagiza walimu na watendaji wa sekta ya Elimu katika ngazi zote kuongeza bidii katika usimamizi na ufuatiliaji wa utoaji wa elimu ili kufikia malengo ya elimu yaliyopangwa na serikali.

 

Latest News

AKAMATWA NCHINI AUSTRIA AKIWA AMEIBA VINYONGA 74 KUTOKA TANZANIA.
27 Jan 2021 07:39 - Grace Melleor

Vinyonga 74 wameokolewa na kupelekwa kwenye bustani ya wanyama ya nchini Austria baada ya kubainika wakiwa kwenye sanduk [ ... ]

RAIS JOE BIDEN AMUONYA RAIS WA URUSI VLADMIR PUTIN
27 Jan 2021 06:39 - Grace Melleor

Rais wa Marekani Joe Biden amemuonya kiongozi wa Urusi Vladimir Putin kuhusu kuingilia uchaguzi wa nchi hiyo.

WANASHERIA WA BOBI WINE WARUHUSIWA KUMUONA MTEJA WAO.
22 Jan 2021 08:40 - Grace Melleor

Jeshi la UPDF na polisi nchini Uganda wamewaruhusu wanasheria wa waliokuwa wa mgombea wa kiti cha urais Robert Kyagulany [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.