Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, amepata nafasi ya hifadhi ya kisiasa nchini Canada.
Wakili wake Lema George Luchiri amethibitishi kuwa familia ya Lema iliondoka jana nchini Kenya akiwa na familia yake, wakili wake George Luchiri Wajackoyah athibitisha.
Mwezi uliopita Godbless Lema alikamatwa na polisi nchini Kenya kwa madai ya kuingia nchini humo kinyume na sheria na kumuachia huru baada ya muda mfupi.
Kwa mujibu wa wakili wake amesema, Lema ambaye alikuwa ameambatana na familia yake na alikuwa akielekea jijini Nairobi kwa ajili ya kutafuta makazi ya muda baada ya kutishiwa maisha.