Mwenyekiti wa Chama cha ACT wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad amepishwa rasmi kuwa Makamu wa rais wa kwanza wa Zanzibar.
Wakati akila kiapo hicho, Maalim Seif ameahidi kushirikiana na rais wa Zanzibar kwa hali na mali ili kuijenga Zanzibar kwa usalama na amani.
Maalim ametoa shukrani kwa wananchi wa Zanzibar na kusisitiza kuwa "imani ya wananchi wangu ndio wito mtakatifu unaonilazimisha kusimama kuwatumikia".
Maalim Seif ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha ACT Wazalendo, amekishukuru chama chake kwa kumpendekeza kuwa Makamu wa Rais wa Zanzibar, na amewataka wananchi wote wa Zanzibar wa ndani na nje, kushirikiana ili kuijenga Zanzibar.
Desemba 6 mwaka huu Rais Mwinyi alimteua Maalim Seif Sharif Hamad kuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Aidha, ameeleza kuwa uamuzi wa yeye Maalim pamoja na chama chake kufikia uamuzi wa kukubali kuingia katika serikali shirikishi ulikuwa mgumu sana ila nia ya rais Dkt.Hussein Mwinyi ndio iliyowafanya wafikie uamuzi huo na kuweka pembeni yaliyotokea hapo nyuma.