Star Tv

Rais wa Zanzibar Dkt.Hussein Mwinyi amemteua Mwenyekiti wa chama cha upinzani ACT- Wazalendo Seif Sharif Hamad kuwa Makamu wa kwanza wa Rais visiwani humo.

Awali akitangaza uamuzi wa kuungana na serikali ya CCM, Katibu Mkuu wa Chama hicho ADO Shaibu alisema uamuzi huo umeridhiwa na kamati kuu ya chama hicho baada ya kutafakari kwa kina. Shaibu alisema uamuzi huo sasa pia utawawezesha Madiwani, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Wabunge kupitia chama hicho, kuweza kushiriki kwenye vyombo vyao vya uwakilishi ili kuendeleza mapambano.

Katika mkutano maalum wa kamati kuu ya chama cha ACT Wazalendo, waliamua kuwa wapendekeze jina la mwanachama atakayekuwa makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar.

Pia ACT Wazalendo, imewaruhusu wajumbe wa baraza la wawakilishi, wabunge, na madiwani waliochaguliwa kukiwakilisha chama na wananchi waliowachagua.

Miongoni mwa sababu walizotoa kufikia uamuzi huo ni pamoja na kutathmini historia ya mapambano ya demokrasia Zanzibar na Tanzania bara kwa ujumla na kusema kuwa mara nyingi matukio ya raia kujeruhiwa, uwepo wa uhasama wa kisiasa, kudhalilishwa kijinsia na mali za watu kuharibiwa yamekuwa yakijirudia huku jambo muhimu ni kuwa na amani.

Aidha, Kamati kuu ya ACT, imeahidi kufanya mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi Zanzibar ili kurejesha imani ya wananchi juu ya uwepo wa uchaguzi huru na wa haki.

Kwa mujibu wa Chama cha ACT Wazalendo, hali ilivyo kwa sasa Zanzibar inahitaji busara kubwa katika kuponya majeraha yaliyotokana na uchaguzi huo, ili kuhakikisha kuwa matukio ya namna hiyo hayajirudii tena.

Katiba ya Zanzibar inasema kuwa Muundo wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar utakuwa wa Umoja wa kitaifa na utendaji wa kazi zake utafanywa katika utaratibu utakaohakikisha umoja unaendelezwa nchini na lengo la kufikia demokrasia.

Hatua ya ACT- Wazalendo kuridhia kujiunga katika serikali ya umoja wa kitaifa, imepokelewa kwa hisia tofauti , wengine wakibeza hatua hiyo, wengine wakiunga mkono kwasababu awali chama hicho kikuu cha upinzani kilikataa kuyatambua matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kwa kusema kwamba yalikua batili.

Baada ya majadiliano ya muda mrefu pamoja na kupokea maoni ya wanachama wake, kimeamua kuungana na serikali ya chama tawala kwa ajili ya kuendesha nchi.

 

Latest News

WANAOGESHA MAGARI BARABARANI HOVYO KUWAJIBISHWA BILA HURUMA.
20 Jan 2021 14:26 - Grace Melleor

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, ameitaka Bodi ya mfuko wa Barabara (RfB) kutumia vifungu [ ... ]

KENYA KUPOKEA DOZI MILIONI 24 ZA CHANJO YA CORONA.
20 Jan 2021 14:06 - Grace Melleor

Kenya inatarajia kupokea dozi milioni 24 za chanjo ya ugonjwa corona iliyotengenezwa na kapuni ya Astrazeneca na chuo ki [ ... ]

BIDEN AJIANDAA KUINGIA IKULU, HUKU TRUMP AKISUSIA KUHUDHURIA KUAPISHWA KWAKE.
20 Jan 2021 08:14 - Grace Melleor

Rais mteule wa Marekani Joe Biden aliwasili Washington katika mkesha wa sherehe ya kuapishwa kwake, wakati mtangulizi wa [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.