Star Tv

Mgombea urais wa JMT kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu amezitaka Jumuiya za Kimataifa pamoja na jumuiya za kikanda ziingilie kati taarifa za matokeo ya uchaguzi wa Tanzania.

Lissu amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari leo Oktoba 29,2020 ambapo ameeleza kuwa Jumuiya za Kimatifa zitoe taarifa za ukweli na Watanzania waingilie kudai haki yao kwa amani kwa njia ya kidemokrasia.

Aidha, Lissu amesema kuwa chama chake kimeweka wagombea 244 wa ubunge nchi nzima, kati ya hao 63 walienguliwa, udiwani 3754 kati yao wagombea 1025 walienguliwa, hivyo takribani 30% walienguliwa.

Mgombea Urais huyo amedai kuwa mawakala wengi wa upinzania hawakupewa barua ya kuingia kwenye vituo vya kupigia kura; "Mawakala waliobaki kwenye vituo hakuna aliyepewa nakala ya matokeo ya uchaguzi kama sheria inavyotaka,hiyo peke yake inathibitisha hakuna uchaguzi wa vyama vingi, hata kwa sheria zetu kama zilivyo huu haukua uchaguzi majimbo yote , kata zote CCM wametangaza ushindi".

Aidha, wakati hayo yakiendelea kubainishwa na Lissu, Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania imekanusha madai hayo ya upinzani na kusema tuhuma zinazotolewa hazijawasilishwa rasmi.

Latest News

RAIS WA CHAD, IDRISS DEBY ATIMIZA MIAKA 30 MADARAKANI.
01 Dec 2020 14:48 - Grace Melleor

Desemba 1, 1990, Idriss Déby alichukua hatamu ya uongozi wa nchi ya Chad kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa, H [ ... ]

“HATUONDOKI CHADEMA, TUNAKATA RUFAA”- Halima Mdee.
01 Dec 2020 13:01 - Grace Melleor

Wabunge 19 wa viti maalum waliovuliwa uanachama wa chama cha upinzani Chadema, wamesema wataendelea kuwa 'wanachama wa h [ ... ]

MTANZANIA ALIYETEKELEZA SHAMBULIZI CHUO CHA GARISSA AJINYONGA GEREZANI.
30 Nov 2020 10:05 - Grace Melleor

Mtanzania Rashid Charles Mberesero aliyehukumiwa kifungo cha maisha mwaka 2019 baada ya kupatikana na hatia ya kushiriki [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.